Tuesday, 31 May 2016

UFUGAJI WA SAMAKI.

UFUGAJI WA SAMAKI.

1.Mambo yakuzingatia wakati wakuchagua eneo kwaajili ya ufugaji samaki.
I. Aina ya udogo: hili nijambo muhimu kwani aina ya udogo huathiri kwenye kuchagua aina gani ya bwawa litumike. Tambua kuwa kuna aina nyingi ya mabwawa kama bwawa la udogo tupu (earthen pond) na bwawa la zege (concrete pond). Bwawa la zege hutumia gharama nyingi kulijenga ukilinganisha na bwawa la udogo tu. Hivyo ili bwawa liwe la udogo ni lazima aina ya udogo wa eneo husika uwe na sifa ya kutunza maji.
II. Maji: samaki huishi kwenye maji hivyo nilazima uwahakikishie upatikanaji wa maji safi na salama kwa uhai wao. Maji yawe yanapatika kwa Wingi, Salama na yenye kuweza kuwekwa katika miundombinu sahihi kwaajili ya kutumika wakati wowote. Maji yanaweza kuwa ya kisima, mto, ziwa, chemchem,au bomba. Kila aina ya maji ina faida zake na changamoto zake. Kwa mfano wakati maji ya mto huwa yanaweza kupatikana kwa urahisi lakin yanachangamoto yakuweza kukuletea vijidudu vya magonjwa kama minyoo, typhoid na kipindupindu.
III. Vifaranga: usishangae! Ndiyo mbegu za samaki yaani samaki wadogo huitwa vifaranga. Nilazima ujihakikishie upatikanaji wa mbegu bora kwaajili ya matokeo mazuri. Mbegu duni huchukua muda mwingi kukuwa na hivyo kumuongezea mkulima gharama za ufugaji na kumpunguzia kipato.
IV. Chakula: ufugaji wa samaki kwaajili ya biashara humuitaji mkulima kuwapatia samaki chakula za ziada (supplementary feed) ili samaki wakue kwa haraka zaidi. Kumbuka ukuwaji wa samaki hutegemea UBORA WA MAJI + UBORA WA CHAKULA.
V. Ulinzi na usalama:  ni vyema mkulima kuepukana na migogoro yeyote kama ya umiliki wa ardhi na matumizi ya maji ili kuondoa uwezekano kukuhujimiwa katika mradi wake.
VI. Usafiri: kwa nyakati tofauti mkulima atahitajika kusafirisha ima malighafi zitumikazo kwenye ufugaji au mazao ya ufugaji baada ya kuvuna. Hivyo ni muhimu kuzingatia uwezekano wa usafiri sahihi wakati wote. Usafiri siyo mtu awe na gari hapana ila uwepo wa miundombinu safi yaweza tosha.
VII.Soko: Mwisho wa ufugaji ni kuuza mazao yako kwa faida hivyo ni vyema mkulima akafanya tafiti za kupata soko la uhakika kwa mazao yake. Mkulima huweza tumia soko la karibu kama majirani na wafanyabiashara wa karibu. Pia anaweza kutumia soko la mbali.

Ufugaji wa samaki unalipa endapo tu mkulima atapata mtaalamu sahihi na akazingatia kanuni za ufugaji.

itaendelea.........................

Soma Zaidi Hapa →

Saturday, 14 May 2016

BUSTANI ZA NYUMBANI.

TANGAZO  TANGAZO  TANGAZO.

ILE KAMPENI YA UFUNDISHAJI WA BUSTANI ZA NYUMBANI NYUMBA KWA NYUMBA BADO INAENDELEA.

ELIMU HII TUNAIFANYIA NYUMBANI KWAKO KWENYE ENEO AMBALO UNAHITAJI KUFANYIA HIYO BUSTANI.

TUNAKUSHAURI KIPI CHA KUFANYA KUTOKANA NA ENEO ULILONALO.TUNAKUPA ELIMU YA NAMNA YA KUUBOLESHA UDONGO WAKO,NAMNA UNAVYOPASWA KUWEKA RESHO YA UDONGO NA MBOLEA,TUNAKUELIMISHA MBOGA GANI YA KUPANDA ILI IWEZE KUWA SEHEMU YA LISHE KWAKO NA BIASHARA PIA.

TUNAKUPATIA ELIMU ITAKAYOKUWA SEHEMU YA KUKUINGIAZIA KIPATO CHA ZIADA.

UNAWEZA KUTAFUTA ELIMU KWA MIAKA 5 BILA YA KUWA NA UJUZI KWA GHARAMA KUBWA.LAKINI HII ELIMU NINAYOKUPA NI UJUZI AMBAO UKIUTUMIA VIZURI INAKUWA NI SEHEMU YA KUKUINGIZIA KIPATO KWA GHARAMA NDOGO SANA.

ILI KUJUA NI NAMNA GANI YA KUPATA ELIMU HII NIPIGIE KWA NAMBA HIZO CHINI ILI UWEKE ODA YAKO LEO AU SMS.

0784 999 995.

0654  768  400.

Soma Zaidi Hapa →

Friday, 6 May 2016

ZAO LA EMBE.

MAEMBE NI UTAJIRI MKUBWA

Waswahili husema eti rizizki ya Mbwa ipo miguuni mwake,usemi huu unamaana kuwa riziki ya mtu ipo katika nafasi aliyo nayo na uwezo alionao
Maembe yaliopo Tanzania yanaweza kubadilisha na kumuongezea riziki ya mkulima wa Tanzania kama akielimishwa vizuri kuhusu ukulima bora na wa kisasa
Maembe yanaweza kumnyanyua mkulima kwa kumuongezea kipato na kuboresha maisha ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi.
Utayarishaji wa shamba la miembe,mkulima anashauriwa kuandaa shamba mapema, kutumia mbegu na miche bora iliyofanyiwa utafiti na vituo vya utafiti hapa nchini.
Mikoa yote inalima miembe ila inatofautiana kwa kiwango cha uzalishaji kutokana na tofauti za maeneo hayo
Zao hili linalimwa katika mikoa yote kwa sababu ya uwezo wake wa kustawi katika aina mbalimbali za udongo na kustahimili aina mbalimbali za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukame.
Miembe inaweza kustawishwa mahali ambapo aina nyingine nyingi za mazao haziwezi kustawi.
Zanzibar ilishazalisha jumla ya Tani 6,546. Kiasi hicho cha embe kilivunwa katika mashamba yenye jumla ya eneo la Hekta 1,372
Ingawa miembe imepandwa Zanzibar katika eneo lenye jumla ya Hekta 1,734 na kaya zilizohusika na kilimo hiki ni 12,819.
Ingawa takwimu hizo hazikuonesha kuwa sasa Tanzani iko nafasi ya ngapi katika uzalishaji wa zao la embe ,
Hata hivyo zinaonesha kuwa kuna ongezako la Tani 146,028 katika kipindi hicho. Ambapo maembe mengi yamezalishwa hapa Tanzinia
Soko la maembe limekuwa kwa kiasi kikubwa duniani ikiwa ni moja ya sababu ya kuongezeka wataalamu wa maembe
Kuna aina zaidi ya 140 za embe ambazo hupatikana hapa tanzania na duniani kwa ujumla kulingana na mazingira yake
.
Ubora wa embe unatofautiana kutokana na sifa za embe na aina ya embe husika ijapokuwa kila embe lina ubora wake.
Sifa hizo zipo nyingi sana, hata hivyo ili kurahisisha kuzitofautisha baadhi ya embe zinazojulikana zaidi katika masoko Tommy Atikns KEITT na kent zill aina hizi ni nzuri sana
Hukomaa mwanzoni hadi katikati ya msimu Matunda yake ni makubwa, huweza kufikia kati ya gramu 450 hadi 700 Umbile la tunda ni kati ya umbile la yai na mviringo
Likikomaa huweza kukaa muda mrefu bila kuharibika Tunda lina rangi nyekundu ambayo haijakolea na imechanganyika na njano na Lina utamu wa kadiri
Zipo aina nyingi za maembe zilimwazo na wakulima hapa nchini kama vile embe dodo, bolibo, sindano, zafarani, mviringa na nyingine nyingi ambazo tumezizoea.
Aina hizo za maembe uzalishaji wake ni mdogo lakini wataalamu wameweza kuingilia kati tatizo la uzalishaji mdogo kwa kutumia mbinu ya ubebeshaji wa maembe.
Ubebeshaji wa maembe ni njia sahihi katika kuhamisha sifa halisi cha maembe kutoka kwenye mche unaotoa mavuno mengi bila kuathiri sifa na tabia za embe unalokusudia kupata.
Mbinu hiyo hutumia shina mama lenye sifa ya kutafuta chakula kwa wingi ardhini na hubebeshwa na aina nyingine inayokidhi mahitaji ya mkulima kwa kumpa bei nzuri.
Matokeo ya utumiaji wa mbinu hiyo ya ubebeshaji wa maembe sasa kuna aina mpya za maembe zinazoweza kupenya soko la maembe la kimataifa.
Aina hizo ni Red, Apple, Alphoncal ambazo tayari zimepiga hodi kwa wakulima wa maembe wa wilaya ya Mkuranga.
Mbali na hayo kuna aina ya miembe inayokidhi sifa hizo ni pamoja na Kent, Keith, Tommy Atkins, Alphonso, Sabre, Van Dyke, Apple, Ngowe na Red Indian (Zill).
Wakulima walio karibu na bustani zinazomilikiwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika pamoja na zile zilizoko chini ya manispaa wameanza kupanda aina mpya za maembe.
Bustani zinazomilikiwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia kitengo chake cha promotion ya mazao zipo Mpiji wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,
Bustani ya Manispaa Ilala yenye aina mpya za maembe ni ile ya Kinyamwezi ambayo ipo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kupitia Gongola Mboto kuelekea njia ya Chanika,Pia zipo nyengine ambazo zipo maeneo ya Lushoto na Muheza Tanga
Wakulima wengi hawajui kanuni bora za kilimo cha maembe na hivyo kuwafanya wakulima kutoyaona manufaa ya maembe
Tatizo kubwa linalo kabili uendelezaji wa zao la embe ni kutopatikana kwa miche ya kutosha ya miembe bora.
Pia bei kubwa ya miche ambayo, huuzwa kati ya shilingi 2,000/= na 3,000/= kwa mche
Ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa miche bora ya miembe Wizara ya kilimo chakula na ushirika imeweka mkakati wa kuongeza uzalishaji wa miche hiyo na upatikanaji kwa wakulima.
Miche hiyo bora ina sifa za kuzaa maembe mengi kwa eneo na yenye ubora unaokubalika katika masoko yetu ya humu nchini na yale ya nje ya nchi.
Wapo wakulima ambao wanawezeshwa kuanzisha mashamba ya miembe bora kwa kupewa miche bora ya miembe na kupanda katika mashamba yao.
Miembe imepandwa katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dodoma na sehemu nyingine hapa nchini.
Mashamba hayo yanakuwa ni mashamba ya mfano ambapo wakulima wanayatayarisha mashamba kwa kufuata kanuni zote za kilimo bora cha miembe.
Mashamba hayo yatakuwa ni sehemu ya kuwafundishia wakulima wengine kwa kuona aina mbalimbali za miembe bora jinsi inavyoweza kuzaa maembe yenye ubora zaidi
Baada ya miaka mitatu miche hiyo itaanza kuwa tayari kutoa vikonyo ambavyo vitatumika kuzalisha miche mingine unaofanywa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika katika kuendeleza zao la embe.
Jumla ya miembe bora 5,141 imezalishwa na kupandwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuwafaidisha wakulima
Miche 595 ya miembe bora imepandwa Dodoma Vijijini huko Chamwino katika Tarafa ya Mvumi na vijiji vake, Makulu miche 200, Ilolo miche 100, Muungano miche 100 na miche 195 ilipandwa Ikowa Dodoma.
Pia Miche 150 imepandwa katika Kituo Cha Amani kijiji cha Makang’wa Dodoma,Miche 120 na kijiji cha mwambaya wilayani Mkuranga
Pia wapo wkulima ambao watagaiwa Miche mingine 400 wilayani Mkuranga namiche 250 itakayo gaiwa Morogoro.
Hata hivyo jumla ya Miche 3,500 ya miembe bora imezalishwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushika kwa kushirikiana na wanachama wa Chama cha Wakulima wa Miembe ili kuwanufaisha wakulima
Miche hii ya kisasa inachukua miaka miwili na nusu kuanzia kupanda hadi kuzaa ile ya zamani inayochukua miaka mitano had saba kupanda hadi kuzaa
Kila mwaka idadi hiyo ya miche itakayozalishwa itakuwa inaongezeka kwa zaidi ya mara mbili Mashamba hayo ni ya wakulima wenyewe ambapo yanakuwa na malengo makuu matatu yafuatayo
Kama wakulima watatilia mkazo kwenye zao hili kwa kutumia mbegu sahihi za maembe zinazo zaa sana na kuchukua mda mfupi wanaweza kuondokana na umasikini
Mkoa wa pwani hivi karibuni uliweza kujionea mradi wa maembe ulikuwa umetembelewa na Raisi Jakaya Kikwete unaomilikiwa na Dkt. Salum Diwani
Shamba lililokuwa limesheheni miembe mingi ya kisasa iliyokuwa imezaa vizuri ilikuwa ni changamoto kwa yeyote alikuwepo kwenye mkutano huo kulima maembe
Iliwekwa wazi kuwa soko la maembe hayo linapatikana nchini Tanzania na nchi za jirani kulinga na ubora wake
Raisi Jakaya Kiwete alitoa changamoto kwa wizara ya kilimo chakula na ushirika kuandaa program maalum kuendeleza kilimo cha maembe katika mikoa inapostawi
Ilikadiriwa kuwa mti mmoja mkubwa wa mwembe huweza kutoa maembe hadi 3000 na midogo hutoa maembe 300
Huu ni utajiri kwani mkulima akilima miti kumi ikazaa vizuri midogo inaweza kuzaa maembe elfu tatu 3000 na mikubwa kutoa maembe elif thelathin 30,000
Hivyo mkulima akiuza embe moja kwa shilingi 300 huweza kupata kati ya 900’000 na 9,000,000 kwa miembe mikubwa na midogo
Mkulima angeweza kufaidika sana na kilimo cha maembe na hata kuitambulisha nchi kimataifa
Kuna mradi ujulikanao kama common Fund for Commodity ambao Tanzania na Zimbabwe ni wanachama na wamepewa furusa ya kuandaa mazao ya biashara ya kuuza nchi za nje
Soko la miembe hapa Tanzania lipo isipokuwa wanunuzi kutoka nje wanahofia kufanya biashara na watanzania kwa kile wasemacho kuwa hawjajipanga kutojitosheleza
Wenyewe
Yupo Inzi ajulikanaye kama inzi maembe kwa jina la kitaalamu bactrocera invadens husababisha funza ambao huharibu maembe
Funza anayejitokeza baada ya mayai kuanguliwa huishi kwa kula nyama ya maembe na kusababisha vidonda ndani ya embe na matokeo yake ni kuoza kwa embe.
Mara nyingi funza huchangia kwa kiasi kikubwa kushusha thamani ya embe na kufanya soko lake kuanguka
Wadudu wanachangia kuharibu soko la embe kutokana na kufanya embe kuoza mapema kabla ya kuiva na kupelekwa sokoni
Wapo wadudu mbalimbali ambao wanaweza kuharibu maembe kama vile Inzi ambao hutoboa na kutaga mayai ndani ya embe na husababisha embe kudondoka mtini
Tuna wakulima wengi wa maembe sehemu nyingi hapa Tanzania kama Kilimanjaro Tanga na hata Morogoro ambapo mda sio mrefu watakuwa na elimu kuhusu kilimo cha maembe
Ijapokuwa sio wakulima wote wana elimu kuhusu kilimo endelevu cha maembe na magonjwa yanayo athiri zao la maembe lakini elimu hawezi kuwa kuta wote kwa wakati mmoja
Watalaam wa Wizara pamoja na wa Halmashauri huvitembelea vijiji mbalimbali na kukutana na serikali ya kila kijiji husika ili kuwaewesha kazi inayokusudiwa kufanyika katika vijiji vyao.
Katika hatua zote ushirikishwaji wa wakulima unazingatiwa ili kukifanya kilimo hiki kuwa endelevu.Ili kutimiza azma hiyo Wizara imekwisha fanya mabo mengi mfano
Wizara imekiimarisha Bustani ya kuzalisha miti ya matunda ya Mpiji huko Bagamoyo pamoja Pampu za maji 5 ambazo zimenunuliwa.
Matenki ya maji 5, moja la lita 3,000 na manne ya lita 2,000 kila moja yamenunuliwa ili kukizi mahitaji muhimu.
Watanzani tuna takiwa kuiga mfano wa Colombia ambayo huwa inapata dola za marekani mill.200 kwa mwaka kwa kuuza maembe Ulaya pesa ambayo kwa Tanzania ni sawa na mazao mawili
Ili kufikia lengo la kukuza soko la maembe kwa, mkulima anatakiwa kupalilia shamba lake pamoja na kusambaza dawa za mda mfupi
mwisho

Soma Zaidi Hapa →

UJENZI WA MABANDA BORA YA KUKU.

KANUNI ZA MSINGI ZA UJENZI WA MABANDA YA KUKU WA NYAMA
KUKU 1,000 - 10,000 (UFUGAJI WA KIWANGO CHA KATI) ...mwendelezo...

[[ Kwa wajasiliamilia wenye mtazamo wa kufanya uwekezaji mkubwa. Mtazamo wa kiviwanda.
Kuwa na uwezo wa kusambaza kuku bora kwa idadi kubwa katika mwaka mzima!
Ufugaji wa kati kitaalamu wenye lengo la kukua kwenda kiwango cha juu (kuku zaidi ya 100,000/=)
Uhitaji wa kuku kwa Dar es Salaam na mikoa mingine ni mkubwa, hasa kuku wa kiwango cha ubora!
Hii ni kwa wale tu wenye maono na wenye kujitoa kwa dhati! Fursa ni yako mpaka soko la kimataifa! ]]

MAMBO YA MSINGI KATIKA SHAMBA LA KUKU
=== Uchaguzi wa shamba
-- Weka shamba sehemu ambayo inaruhusiwa kisheria kwajili ya ufugaji (Ofisi za ardhi halmashauri zitakusaidia)
-- Nunua shamba kwa kufuata taratibu za kisheria na uwe na umiliki halali wa kisheria
-- Hakikisha shamba lako ni kubwa la kutosha huku ukizingatia upanuzi wa siku za mbeleni
-- Chagua eneo ambalo jumla ya gharama za uzalishaji zitakuwa ndogo zaidi (malighafi na wafanyakazi)
-- Ni vyema sana shamba lako liwe jirani na soko ili kupunguza gharama za usafiri
-- Chagua eneo ambalo malighafi za uzalishaji zinapatikana (maji, chakula…)
-- Ni vyema shamba lako liwe sehemu ambayo maji hayatuami, kama si hivyo basi uboreshaji wa kitaalamu ardhi ufanyike
-- Shamba liwe katika sehemu ambayo mabanda yataweza kupata hewa nzuri na safi
-- Ni vyema shamba lako liwe mbali na makazi  na shughuli za watu
-- Chagua eneo ambalo litakuwa na ulinzi na usalama (maeneo ambayo hayana migogoro, vibaka…)
-- Hakikisha kuwa shambani mwako umeweka mifumo ya kudhibiti majanga ya moto

=== Maboresho ya shamba
-- Dhibiti mmomonyoko wa ardhi kwa njia stahiki
-- Hakikisha kuwa eneo lako lipo juu ya kiwango cha maji ya mafuriko ya eneo hilo
-- Yatengenezee maji mtiririko mzuri ili yasituame na uyaelekezee katika njia inayofaa
-- Kama eneo linatuamisha maji, basi waweza kulinyanyua juu kwa mawe na kifusi
-- Panda ukoka na boresha mandhari iwe ya kupendeza
-- Upande ambao utakuwa una mwonekano mbaya, waweza kupanda miti ili kuukinga
-- Hakikisha kuwa shamba lako limezungukwa kwa usalama wa kutosha
-- Ni vyema shamba lako likiwa na wigo uliozunguka pande zote na geti la kuingilia
-- Wigo wako uwe imara kuhakikisha kuwa wanyama hawachimbi chini na kupita
-- Tengeneza barabara ya kuingilia inayotosha katika kiwango cha kitaalamu huku ukifuata taratibu na sheria
-- Ondoa vichaka, fukia mashimo hatarishi ya eneo hilo n.k
-- Ondoa vishawishi vyote vya mwewe, nyoka n.k.
-- Dhibiti wanyama kama nyoka, mwewe na jamii hiyo

=== Mpangilio wa ndani wa shamba
-- Kuwa na shamba kubwa la kutosha shughuli zote huku ukizingatia upanuzi wa siku za mbeleni
-- Fahamu idadi ya kuku utakao fuga huku ukizingatia upanuzi wa baadaye
-- Idadi ya mabanda, aina ya nyumba zitakazo hitajika zitategemea idadi ya kuku na namna ya mfumo wa kuendesha mradi wako
-- Shamba lipangiliwe kwa namna ambayo kutakuwa na mtiririko mzuri wa shughuli na nafasi ya kutosha
-- Mpangilio wa shamba uruhusu nafasi ya kupita vifaa kati ya banda moja na jingine
-- Hakikisha kuwa mabanda yamekaa kwa namna na nafasi ambavyo magonjwa hayataweza kusafiri toka banda moja kwenda jingine
-- Mabanda yatazame upande ambao utahakikisha kuwa kipindi cha joto hewa na upepo mzuri unaweza kuingia na kupooza
-- Mabanda yakae upande ambao ni huru na viatalishi kama magonjwa, shughuli za binadamu n.k.
-- Hakikisha kuwa shamba lako limepangiliwa kwa namna ambayo magari yataweza kugeuka na kukata kona
-- Eneo la kutupa taka liwe upande ambao halitaathiri afya ya binadamu na kuku
-- Hakikisha kuwa utupaji taka na utumiaji madawa hauathiri vyanzo vya maji, ardhi na mazingira kwa ujumla
-- Dhibiti harufu na  kelele shambani mwako ili zisiathiri majirani
-- Baadhi ya kazi zifanyike muda mzuri ambao hautaathiri majirani
-- Shughuli za binadamu zisiathiri afya ya kuku
-- Baadhi ya nyumba utakazo hitaji ni mabanda ya kuku, mabanda ya kuku wagonjwa, mabanda ya kuku wapya, stoo ya chakula, stoo ya vifaa vya kufanyia kazi, karakana, maabara, ofisi, nyumba ya kulala wafanyakazi na meneja, jiko, vyoo, sehemu ya kuhifadhi magari, banda la kuweka lita iliyokwisha tumika, sehemu ya kudhibiti mizoga ya kuku, sehemu ya kuweka matanki ya maji n.k
-- Hakikisha mradi wako unajitegemea humo humo bila kuhitaji vitu vingi kutoka nje ili kupunguza gharama za uzalishaji na vihatarishi

=== vipimo, umbo na msingi wa banda
-- banda lenye umbo la mstatili ndilo ambalo mara nyingi hutumika sana
-- ukubwa wa banda unategemea idadi ya kuku na shughuli ambazo zitakuwa zinafanyika ndani
-- kwa kuku wa nyama, mita moja ya mraba wanakaa wastani wa kuku 10
-- msingi wa banda unapaswa kuwa imara kubeba uzito wa banda
-- aina ya msingi ujengwe kutegemea na ushauri wa Mhandisi husika
-- piga dawa ya wadudu kwenye msingi kuzuia mchwa na wadudu wengine
-- zuia unyevu kuja sakafuni kwa kutumia DPM
- sakafu ya banda iwe ya zege kuhakikisha uimara, ugumu na kuzuia zaidi unyevu
--hakikisha msingi umenyoka na pima maji
-- kinga msingi na mmomonyoko wa ardhi
-- kama banda litajengwa kwa nguzo, basi hakikisha zimewekwa na kushikwa vizuri katika msingi

=== kuta, madirisha, milango, paa
-- kutegemea na aina ya kuta utakayotumia, hakikisha imejengwa sehemu stahiki, imara kuhimili mizigo yote
-- kimo cha kuta kiwe chenye kuruhusu shughuli kufanyika ndani ya banda na chenye kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa
-- ndani ya banda kuta ziwe laini ili ndege wasijiumize
-- hakikisha kuta zinakiwango cha kutosha cha mpitisho wa joto
-- hakikisha kuta zinauwezo wa kuzuia unyevu
-- weka milango kulingana na uhitaji huku ukizingatia kutoathiri shughuli za banda huku ukihakikisha uimara, ulinzi na usalama
-- weka madirisha yenye ukubwa wa kutosha yenye kuwezesha upepo kupita juu ya kuku
-- tumia nyavu zinazostahili katika madirisha kuweka usalama, ulinzi na udhibiti unaostahili
-- funika madirisha na mapazia maalumu yenye mfumo wa kufunika na kufunga dirisha ili kuruhusu kiasi maalumu cha upepo kupita
-- mapazia yawe yenye kufunika vizuri kuzuia kabisa upepo usiostahiri kupita
-- weka vidirisha vya kupitisha upepo juu mwisho wa kuta kuruhusu upepo wa baridi kuingia ndani kulingana na usanifu wa kitaalamu
-- paa liwekwe lililo imara na kuhimili mzigo
-- ni vyema zaidi upana wa jengo uwe huru bila kizuizi katikati
-- ulalo wa paa uwe mzuri kuruhusu kumwaga maji na kubeba mzigo
-- paa lishikishwe vizuri katika nguzo/ukuta kuhakikisha usalama
-- paa liwe na kiwango maalumu cha mpitisho wa joto
-- paa liweze kuzuia unyevu
-- paa lipitilize nje zaidi ya kuta kuzuia maji ya mvua na jua kuingia ndani ya banda
-- kwa mabanda yaliyo mapana zaidi ya mita 8, madirisha ya kupitisha na kupooza hewa  juu paani ni ya muhimu
-- madirisha ya juu paani yafunikwe vizuri kuhakikisha kuwa wadudu, ndege, wanyama na maji hayapiti
-- banda linaweza kuwa na vyumba vya ndani kulingana na uhitaji
-- hakikisha kuwa jengo zima ni imara
-- jengo lote liwe zuri na lenye kuvutia ndani na nje
-- jengo liwe limesanifiwa kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa

=== nyenzo za ujenzi
-- Msingi: mawe, tofali, zege
-- kuta: mawe, tofali, zege, mbao, miti, mabanzi, EPS panels, bati, Superflex, turubai
-- paa: mbao, chuma, bati, turubai, superflex, EPS panels, vigae, nyasi, makuti.

Soma Zaidi Hapa →

MAGONJWA YA NYANYA.

MAGONJWA YA NYANYA DALILI NA UTHIBITI WAKE.


1.Dalili za madoa yatokanayo na bakteria hutokea kwenye majani, matawi na kwenye

matunda ya nyanya. 

DALILI
Dalili bayana zaidi huonekana kwenye majani, ndio maana ya hilo jina ‘Madoa ya majani kutokana
na bakteria’. Makovu madogo ya rangi ya manjano-kijani hujitokeza kwenye majani machanga na
matokeo yake ni majani yaliyopindapinda, yaliyokoza, yaliyotota na yenye kuonesha ishara kama
yenye mafuta kwenye majani yaliyokomaa.

Makovu hukua haraka na yanaweza kufikia ukubwa wa 0.25-0.5 sm, huwa na rangi ya
kahawia/nyekundu. Umbo la makovu kwa kawaida huwa na pembe kwa vile hufuata umbile la
mishipa midogo ya majani. Makovu mara nyingi hutokea kwenye ncha na pembezoni mwa jani
ambamo unyevu huhifadhiwa. Katika hali ya ujoto/ukavu, majani huonekana yamechanika
chanika kutokana na maeneo ya pembezoni mwa majani na kati ya makovu hukauka na kukatika.

Ukubwa wa makovu huongezeka kutokana na muda ambao majani yanakuwa na maji. Kwenye
matunda, madoa huanza kwa kuwa na rangi ya kijani kibichi na kuonyesha sehemu kama

1: Madoa kutokana na Bakteria (Bacterial spot) (Xanthomonas
zilizotota maji. Kwa kawaida hufikia ukubwa wa 0.5 sm. Madoa haya hatimaye huwa yenye
mnyanyuko, rangi ya kahawia na yenye kukwaruza kwenye tunda la nyanya. Madoa haya kawaida
hufanya njia za kupenya aina nyengine za ukungu na bakteria wavamizi na kusababisha kuoza kwa
matunda.

UDHIBITI
Madoa ya majani yanayosababishwa na bakteria yakishaingia tu shambani au kwenye jengo la
kuoteshea mimea ni vigumu kuyadhibiti. Mbinu zifuatazo zinaweza kuchukuliwa kudhibiti
ugonjwa huu:

Mbinu bora za kilimo

Mbegu zisizo na vimelea vya magonjwa.Miche isiyo na magonjwa .Mzunguko wa mazao.Epuka maeneo yaliyopandwa nyanya kwa muda wa mwaka mmoja.Tumia miche iliyopasishwa.Ondosha shambani na choma moto mabaki ya mimea iliyoathirika na masalio.Safisha na kuua vimelea vya magonjwa katika vitalu kabla ya kusia mbegu.
Matumizi ya kemikali: Madoa yanayosababishwa na bakteria yanaweza kudhibitiwa kwa kutumia
kemikali zifuatazo; Acibenzolar (Actigard 50WG) Copper fungicides (Champ Dry prill, Champ
Formula 2, Copper-Count-N, Cuprofix MZ Disperss, Kocide, Kocide DF, Nordox, Tofix Dispress
Basic Copper) Copper/ EBDC/Zoxamide Mixtures, Cuprof ix Dispress MZ, Gavel, Mankocide)
Famoxadone/Cymoxanil (Tanos) na Streptomycin (Agri-strep).

Kibaiolojia: Virusi vinavyoshambulia bakteria hudhibiti magonjwa haya, lakini ni lazima viwekwe
shambani wakati wa jioni angalau mara mbili kwa wiki. Bakteria wa jamii ya Xanthomonas ambao
hawasababishi magonjwa hutoa udhibiti wa kiasi wa madoa yanayosababishwa na bakteria.

2: Mnyauko kutokana na bakteria (Bacterial wilt)


DALILI

Dalili za awali ni kunyauka kwa majani ya kwenye ncha. Baada ya siku mbili dalili hii huwa ni ya

kudumu, na mti wote hunyauka na kufa kutokana na kuendelea kwa ugonjwa. Matawi yote

hunyauka kwa wakati mmoja. Shina la mti ulionyauka likikatwa shehemu ya kati huwa na rangi

nyeusi na huonekana kama iliyotota maji. 

Shina linapokamuliwa, hutoa maji ya utelezi kijivujivu unaotiririka. Hatua zinazofuata za ugonjwa huu ni kuoza kwa sehemu ya kati ya shina na hii husababisha uwazi katika sehemu hiyo. 

Mzizi ulioathirika huoza na kuwa na rangi ya kahawia mpaka nyeusi. Mnyauko wa bakteria hausasababishi madoa kwenye matunda. Mmea hunyauka ukiwa na rangi ya kijani, (majani hayawi ya njano au kuwa na madoa) na inaweza kutokea ghafla.

Katika hali ya ugonjwa kusambaa taratibu, mti hutoa mizizi mingi juu ya shina na mmea hudumaa.

Kuanguka kabisa kwa mmea hutokea wakati nyuzi joto zinapofikia 320C au juu ya hapo.

UDHIBITI

Mnyauko unaosababishwa na bakteria unaweza kutambuliwa shambani kwa kukata sehemu ya

chini ya shina urefu wa 2-3 sm na kuisimamisha kwenye glasi ya maji. Ikiwa ugonjwa upo, basi

michirizi ya bakteria kama nyuzi hutoka kwenye kipande hicho cha shina sekunde chache tu baada

ya kukisimamisha kwenye maji.

Mbinu bora za kilimo

Mzunguko wa mazao na yale ambayo hayaathiriki.Usipande nyanya katika udongo ambao ugonjwa huu uliwahi kuwemo.Tumia aina za mbegu zenye kustahimili/zisizopata ugonjwa wa mnyauko bakteria. (Kama vileFortune Maker, Kenton na Taiwan F1).Toa na angamiza mimea iliyonyauka kutoka shambani kupunguza usambaaji wa maradhi.Ruhusu mafuriko yenye kuenea.Ongezea mbolea ya samadi.Panda katika msimu ambao si rafiki kwa ugonjwa huu.Zuia minyoo fundo (root-knot nematodes) kwani husaidia uingiaji wa ugonjwa.Changanya na mazao jamii ya kunde.Epuka kutumia ardhi kwa miaka 3-4 baada ya uzalishaji wa nyanya.

Kemikali: Mnyauko wa Bacteria unaweza kudhibitiwa kwa kutumia Chlorothalonil (Bravo

720/Ensign, Bravo Ultrex, Bravo Weather Stik, Echo 720, Echo 90DF, Echo Zn, Ridomil/Bravo).

Juu ya hivyo, tahadhari inapaswa ichukuliwe kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa, hivyo mbinu

ya matumizi ya kemikali katika kuzuia ugonjwa inabidi ichanganye na mbinu nyinginezo.

Kibaiolojia: Kuzuia kunyauka kunakosababishwa na bakteria kunajumuisha matumizi ya ardhi

zenye kuzuia ugonjwa na ardhi zenye vimelea wapinzani (km. Candida ethanolica, Pythium

oligandrum).

2. Yanayosababishwa na Ukungu


DALILI

Dalili za ukungu mapema hutokea kwenye matunda, shina, na majani ya nyanya. Majani huonesha

madoa ya kahawia iliyokoza na yenye mfumo wa duara zenye kati moja. Madoa kwanza hujitokeza

kwenye majani yaliyokomaa na kuendelea juu ya mmea. Majani yenye madoa huweza kufa kabla ya

wakati wake na kusababisha kupukutika mapema kwa majani, matunda huungua kwa jua na kuwa

na rangi isiyopendeza.

Madoa ya kwenye matunda hujitokeza kwa juu kwenye ncha ya shina. Kwa kawaida madoa huwa

na rangi ya kahawia iliyokoza mpaka nyeusi, yaliyozama ndani, magumu na yenye duara za kipekee

zenye mfumo wa kati moja. Kuoza kwa chini ya shina huweza kutokea kwenye miche michanga. 

Hali hii hujionyesha kwa kuzunguka shina sehemu ya chini. Miche iliyoathirika hudumaa na huweza

kunyauka na kufa. Miche mikubwa iliyoathirika huwa na makovu ambayo kawaida huwa upande

mmoja tu wa shina na hurefuka na kudidimia kwenye mashina na vikonyo. Dalili za ugonjwa wa

ukungu mapema mara nyingi hudhaniwa kuwa ni ukungu chelewa, lakini kwenye ukungu chelewa

makovu yamefifia, madogo na hayana alama za duara zilizonyanyuka.

UDHIBITI

Ukungu mapema unaweza kubainika shambani kwa kutafuta madoa ya kahawia iliyokoza ya kiasi

cha 1.2 sm kwa upana. Ni vigumu sana kuzuia ukungu mapema ukishaanza shambani. Njia

muhimu ya kudhibiti ukungu mapema ni kuzuia kuingia kwake na kusambaa.

Mbinu bora za kilimo

Zungusha mazao ya nyanya na nafaka ndogo ndogo, mahindi au jamii za kunde.Panda aina zenye kustahimili ‘early blight’. (Km. Floradade, Hytec 36, Julius F1 na Zest F1).Tumia mbegu safi.Limia na kufukia mabaki ya mazao baada ya mavuno na choma moto mazao yaliyoathirika natakataka zote za mazao.Epuka kumwagilia kwa juu.Ongezea mbolea ya samadi.Tumia matandazo kuzuia kurukia kwa maji.Hakikisha kupanda kwa nafasi sahihi na kufunga vijiti.Toa majani ya chini yaliyoathirika ili kuboresha mzunguko wa hewa.Epuka kutumia ardhi kwa angalau miaka 2 baada ya uzalishaji wa nyanya.

Kemikali: ‘Early blight’ inaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu Boscalid ( Endura

Captan, Captan 4F, Captan 50), dawa za ukungu zenye shaba (Champ Dry Prill, Champ Formula 2,

Copper-Count-N, Kocide 101, Kocide DF, Kocide 4.5LF, Kocide 3000, Nordox Tri Basic),

Chlorothalonil na Chlorothalonil Mixtures (Bravo 720/Echo, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo

Weather Stik, Echo Zn, Ridomil Gold/Bravo), EBDC, Copper FBDC na EBDC/Zaxamide (Cuaprofix Disperss M2, Dithane/Gavel, Maneb 75, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone+Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, Reason 500SC, Penthiopyrad,

Fontelis, Pyrimethanil, Scala), Strobilurin na Strobilurin Mixtures (Cabrio, Flint, Quadris)

Kibaiolojia: Kuna mazao mengi yatokanayo na mimea ambayo husemekana kuwa na sifa za sumu

kwa aina nyingi za ukungu. 

Haya ni mazao asilia ambayo hupoteza nguvu zake haraka juu ya majani na kwenye udongo. Juu ya hivyo, taarifa kidogo sana zinajulikana kuhusu viwango vyao vya matumizi, athari zao juu ya viumbe marafiki, na binadamu.

4: Ukungu Chelewa (Late blight)

DALILI

Dalili za ukungu chelewa hujitokeza kwenye matunda, majani, shina na matawi. Kwenye majani

madoa ya kijani kibichi/kahawia hujitokeza upande wa juu wa majani, na pembezoni mwa

majani huwa kijani kibichi na huwa kama iliyotota, kwa kawaida madoa hutanuka ghafla hadi

majani yote yanapokufa. Nyakati za hewa ya unyevu, ukungu mweupe/kijivujivu hujitokeza

kwenye kingo za madoa katika sehemu za chini za majani. Wakati wa joto, sehemu

zilizoathirika huonesha kukauka. Madoa ya kahawia na yaliyorefuka hujitokeza kwenye

mashina.

Kwenye matunda, madoa ya kijivujivu/kijani yaliyotota hujitokeza kwenye nusu ya tunda

upande wa juu. Madoa haya baadae husambaa na kugeuka kahawia, yaliyokunjamana na

magumu. Wakati wa hali ya unyevu ukungu mweupe hujitokeza kwenye sehemu za matunda

yaliyoathirika. Dalili za ukungu chelewa mara nyingi hudhaniwa ni ukungu mapema (Alternaria

solani), lakini dalili za ukungu mapema mara nyingi huwa za duara zaidi, kubwa, na zilizokoza

na za duara zenye kati moja. Ukungu chelewa hauna duara hizi.

UDHIBITI

Nyanya zilizoambukizwa huweza kushambuliwa kwa haraka na kuteketezwa na ukungu

chelewa. Kuzuia ugonjwa huu ni shida sana ukishajiimarisha shambani. Njia muhimu sana ya

kuzuia ukungu chelewa ni kuhakikisha haijajiimarisha na kusambaa. Hii inaweza kufanyika

kwa kutumia mbinu zifuatazo:

Mbinu bora za kilimo

Zungusha mazao mengine kwa miaka 3 hadi 4.Tumia aina zenye kustahamili ugonjwa huu (km. Meru, Tengeru 97 na Shengena).Tumia mbegu safi.Ondoa mabaki ya mazao na choma moto mimea iliyoathirika na mabaki ya mimea.Tumia moto au mvuke kuua vimelea katika maeneo yaliyoathirika.Weka matandazo ya nyasi kuzuia kurukia kwa maji.Tumia zana safi baina ya mashamba.Hakikisha maji hayatuami na kuwe na mzunguko mzuri wa hewa.Toa majani ya chini yaliyoathirika kusaidia mzunguko mzuri wa hewa.Hakikisha kupanda kwa nafasi inayotakiwa.

Kemikali: Ukungu chelewa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu za aina ya

mrututu (Champ Dry Prill, Champ Formula 2, Copper-Count-N, Kocide 101, kocide DF, Kocide

4.5LF, Kocide 3000, Kocide 6000), Cholorothalolin na Cholorothalonil Mixtures (Bravo

720/Echo 720, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo Weather Stik, Echo Zn, Ridomil

gold/Bravo),EBDC, Copper EBDC/ Zoxamide (Cuprofix MZ Disperss, Dithane, Gavel, Maneb

75 DF, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone +

Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, eason 500SC) Strobilurin na Strobilurin Mixtures ( Cabrio

Flint Quadris).

Kibaiolojia: Mpaka hivi sasa hakuna dawa ya kibaiolojia inayo weza kudhibiti/kuzuia ukungu

chelewa.

Kadi 4: Ukungu Chelewa (Late blight) (Phytophthora infestans)

Kadi 5: Mnyauko kutokana na Ukungu

Soma Zaidi Hapa →

UHITAJI NA UMUHIMU WA MAJI KWENYE KILIMO.

UMUHIMU WA MAJI UNATUPEREKEA KUWEKEZA NGUVU ZETU KWENYE UCHIMBAJI WA KISIMA.     Asilimia 80 ya uhitaji mkubwa wa mazao mengi ni maji na moja ya changamoto kwenye kilimo ni maji. Mfumo huu wa umwagiliaji umetengenezwa kupunguza tatizo hili kwa asilimia kubwa sana kama nitakavyoelezea baadae kidogo.
Utangulizi.
Mfumo wa umwagiliaji wa matone (Drip irrigation system) unafanya kazi kama zile drip za hospital za kuongezewa maji au damu ambazo huwa tunaziita drip... wanasemaga mtu katundikiwa drip ya maji.
Vitu vinavyotengeneza mfumo huu.
1. Pump... Hii inafanya kaza ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kupeleka shambani direct au kwenye tank au water resevour kwa kuhifadhi
2. Filters/ chujio... Filter zinachuja maji ili takataka na particles nyingne siziingie kwenye mfumo wa umwagiliaji na kuleta shida kama za kuziba pipes na emmiters
Emmitters ni visehemu vya kutolea maji kwa ajili ya kumwagilia
3. Back wash controller/ back flow contorller ni vivalve vinavyozia maji kurudi nyuma ya mfumo hasa mgandamizo wa maji ( pressure) inapokuwa ndogo. Maji yanatakiwa yawe na uelekeo mmoja tu (Unidirection). Hizi ni kama valves za mishipa ya vein zinavyozuia damu isirud nyuma
4. Pressure regulator au control valve... inafanya kaz ya kucontrol pressure ya maji inayoingia kwenye pipes... ni muhimu sana kuregulate pressure maana ikizidi tu unaweza kukuta sio drip tena ila pipes au tape zimeburst zote ukazimia😊
5. Water tank/resouvr au chanzo cha maji... kazi ni kusupply maji kwenye drip... lazima maji yawepo ndio uwe mfumo wa umwagiliaji
6. Main line/ pipe ni bomba kubwa linalotoa maji kwenye tank au kwenye source nyingine kwenda shambani kwa ajili ya kusambazwa. 7.Small poly tubes/tapes hizo ndio zileee zinasambaza maji shambani sasa na ndio zenye vitobo vya kudodondoshea maji sasa
Kuna connectors pia ambazo zinaunganisha hizo tubes na pipes
Pia kuna gate valves... hizi zinasaidia kumwagilia shamba kwa awamu... yani unaweza kumwagilia nusu shamba kwanza ukaendelea na nusu baadae. Gate valves Ikifungwa zinazuia maji kwenda eneo moja na kuruhusu eneo jingine hasa kama maji yana pressure ndogo
Kuna source ya power kama umeme au solar kwa ajili ya pump lakin pia unaweza kutumia mafuta tu
Naombeni niendelee na faida za kutumia mfumo huu wa umwagiliaji.
Matumizi mazuri ya maji
Mara nyingi wakulima hawajui kama kumwaga maji hovyo ni tatizo as long as yapo😊. Sasa drip inapunguza kupotea maji unnecessarily kwa sababu inadondosha maji kwenye mmea tu
Kwa wenzangu wa kanda ya kati ambao kuna shida ya maji wataelewa kirahisi au kama unatumia ya DAWASCO yanye mita mtaelewa zaidi😂😂😂
2. Kwa sababu mfumo huu unamwagia maji kwenye shina la mche tu... unasaidia sana kupunguza shida ya magugu shambani... wakat mmea unapata maji tena ya kutosha magugu yanalala njaa😊😊😊 inapunguza usumbufu na gharama za palizi
Ukimwagia kienyeji kwa sababu unamwaga maji mengi kwa wakat mmoja... yanapotea haraka sana na mengine ndio yanaenda kustawisha magugu
3. Matumizi mazuri ya mbolea... hapa patamu😋😋😋
Kwa mbolea za dukani zinazoyeyuka kwenye maji... water soluble...unaziweka kwenye tank zinayeyuka (kutengeneza solution) na then zinaenda kwenye mimea kwa kupitia matone yanatoka kwenye tubes... once again magugu yanalala njaa 😂😂😂. Tofauti na kumwaga shimon then unamwaga lita 5 za maji mbolea inayeyuka na kupoletlea pembeni magugu nayo yanasherehekea😊
4. Haki sawa kwa kila mmea.
Mfumo wa umwagiliaji wa matone unatoa kiwango sawa sawa cha maji na mbolea kwa mimea yoooote shambani. Yami mmea ambao upo karibu na chanzo cha maji unapata kiasi cha maji sawa sawa na mmea ambao upo hukooo mwisho wa shambani... kwa sababu hii basi mazao yanatoka mengi uniform kama matikiti mengi yanakua makubwa na yanayokaribiana sana size.
Tofauti na umwagiliaji wa kawaida ambapo mmea karibu na kisima ndio umapendelewaaa halafu ile ya kwenye margin inakonda kwa sababu watu wanachoka sana pia kubeba ndoo nenda rudi
5. Inapunguza gharama ya nguvukazi na kupunguza chamhamoto ya nguvu kazi
Watu wengi wanaishi mjini wana mashamba bush na vijana wanawadanganya sana kuwa wamemwagilia kumbe sio au wamemwagilia kwa kumbe wamerashia tu... hii system kwa sababu ni ya kufungua tu na kufunga bomba hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kuelekezwa kufungua na kufunga bomba kama ina kijana wa kazi safi angalau kwa sababu hatumii nguvu kubwa sio rahisi kukudanganya
5. Mfumo wa drip unapunguza trembling/ kukanyaga kanyaga shamba ambapo kunasababisha compaction ya shamba na kupunguza circulation ya hewa ardhini
6. KUONGEZA UZAAJI.
Nimeandika kwa herufi kubwa kabisaaaaaa....
Drio irrigation bwana inaongeza uzaaji almost 3-4 times normal irrigation... natumia kwenye matikiti maji... kwa kawaida nilipata tani 4 kwa heka na tani 12 kwa drip. Hii inasababishwa na usawa kwenye maji na mbolea
7. Drip zinapunguza mmomonyoko wa ardhi... tofauti na kumwagilia kienyeji au kwa mitaro
Yan kama unatumia drip na ukaweka matandazo ya plastic (Plastic mulch) umemaliza... no palizi... no energy... high yield... grt production
Pia mfumo wa drip ni portable ambao unaweza kuutumia hata kwenye shamba la kukodi na kuutoa unaweka kwenye kirikuu mpaka home... kuwe na chanzo kizur cha maji tu
Diadvantages
- Mfumo huu ni ghali kidogo hawa kwa wanaoanza kwa sababu roll moje ya mita 2000 inauzwa 1.8M mpka 3.6 ambayo inatosha heka moja tu ya matikiti maji... japo otakisaidia sana kuweka mbegu nyingi shambani na kuvuna sana sana sana
Disadvantage nyingne ni kwamba installation yake inahitaji utaalami kidogo kitu ambacho kinaongeza gharama kwa sababu sio kila mtu anaweza kufunga drip
Kiufupi initial capital inakuwa kubwa sana!.              kwa maelezo zaidi.wasiliana nami kwa namba.                      0784  999  995./0654  768  400.

Soma Zaidi Hapa →

Monday, 2 May 2016

KILIMO CHA MIPAPAI.

MUONGOZO WA UZALISHAJI WA PAPAI
UTANGULIZI
Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.
KUHUSU MPAPAI
Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu
i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya)
Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.
Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI
Miche ya mpapai
Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: -
1. Mbegu za Kawaida (Local seeds)
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.
2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaoja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1, MALAIKA F1 n.k.
Upandaji
Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.
Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.
Kitalu cha mipapai
BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5.
Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi.
Kiaisi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda. Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yalioja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu.
Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI WA SHAMBA
Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba.
Nafasi
Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.
Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.
NB: Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekari ( 400 hadi 800 kwa ekari)
Kupanda mimea shambani
Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.
shamba la mipapai
Uwekaji wa mbolea.
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbole gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phospate kwa kaisi kikubwa. Mfano; - 12:24:12. (NPK)
Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK)
Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.
Umwagiliaji
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji niya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.
Magugu
Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.
HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI
Kitalu - Wiki 1 - 6
Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa shamba - wiki 7 -16
Maua na kuweka matunda - wiki 17 - 21
Kukua kwa matunda - 22 - 26
Mavuno ya kwanza - Wiki 37 nakuendelea.                             KWA MAHITAJI YAKO YA MBEGU HIZI ZA KISASA WASILIANA NAMI KWA NAMBA HIZO CHINI.KWA WA MIKOANI TUNAWASAFISHIA.                  HUSISAHAU PIA KUNUNUA VITABU VYETU CHA BUSTANI ZA MBOGA NA MATUNDA PIA CHA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI PAMOJA NA UCHIMBAJI WA KISIMA CHA KARATI NA UTENGENEZAJI WA GREENHOUSE.                     0784  999  995.                           0654  768 400.

Soma Zaidi Hapa →

Jiunge Nasi Facebook

Zilizosomwa Zaidi

Pages

Powered by Blogger.