Wednesday, 27 April 2016

UFUGAJI WA NGURUWE.

UFUGAJI WA NGURUWE
Nguruwe ni mnyama asiecheua na mwenye kwato zilizogawanyika.

AINA ZA NGURUWE (BREED)
i) Largewhite
-Rangi nyeupe
-Masikio yao yamesimama wima
-Wana miili mikubwa
-Ni wazazi wazuri
-Hutoa nyama nzuri
ii) Landrace
-Rangi nyeupe
-Masikio yao yamelalia mbele
-Mwili mrefu
-Wana nyama nzuri
-Ni wazazi wazuri
iii) Saddleback
-Rangi nyeupe na baka jeusi mgongoni au rangi nyeusi na baka jeupe mgongoni
-Wana masikio yaliyolala
-Ni wazazi wazuri
-Wanatoa nyama nzuri

FAIDA ZA NGURUWE KWA UJUMLA
-Hutoa nyama nyeupe ambayo ni nzuri sana kwa binadamu
-Ni rahisi kutunza kwani wana uwezo wa kula mabaki ya vyakula
-Huzaa kwa wingi na kwa muda mfupi
-Hutoa mbolea kwa ajili ya kilimo
-Hutoa mafuta kwa ajili ya kupikia n.k

AINA ZA UFUGAJI
-Ufugaji wa ndani
Nguruwe hufugiwa kwenye banda tu 100% bila kutoka nje
-Ufugaji wa nje
Nguruwe kufugiwa nje kwa muda mwingi 70%-80%
-Ufugaji wa ndani na nje
Nguruwe kufugiwa ndani ya banda na nje kwenye uzio/fence @50%.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE
-Upatikanaji wa soko kwa ajili ya mazao ya nguruwe
-Aina ya nguruwe unaotaka kufuga kulingana na lengo
-Mtaji kwa ajili ya kuendesha mradi
-Eneo zuri la kuwafugia
-Upatikanaji wa chakula cha kuwalisha
-Utaalamu

VYAKULA VYA NGURUWE NA ULISHAJI
Utunzaji na ulishaji wa nguruwe  umegawanyika katika makundi
-Nguruwe wadogo/watoto
-Nguruwe wanaokua
-Nguruwe wenye mimba
-Nguruwe mzazi au anaenyonyesha
-Nguruwe dume
VIINI LISHE VINAVYOTAKIWA KWENYE CHAKULA CHA NGURUWE
-Wanga (kuupa mwili nguvu)
Pumba za mahindi au mpunga
-Protini (kujenga mwili)
Mashudu aina zote na unga wa dagaa
-Madini
Chokaa, chumvi na pigmix/pigboost
-Vitamini
Majani au mbogamboga
-Maji ni muhimu sana kwa kila kiumbe hai
BAADHI YA MAGONJWA  YANAYOWAPATA NGURUWE NGURUWE
i) African Swine Fever (homa ya nguruwe)
Huu ni ugonjwa hatari sana kwa nguruwe unaosababishwa na virus
ii) Swine dysentery
Huu ni ugonjwa wa kuhara husababishwa na bacteria aitwae treponema hyodyseteriae
iii) Respiratory disease
Ugonjwa wa mapafu
iv) Sarcoptic mange
Ugonjwa wa ngozi husababishwa na mangemites
v) Calibasilosis
Kwa nguruwe wadogo husababishwa na E.coli bacteria
vi) Coccidiosis
Kwa nguruwe wadogo
vii) Erysipelas
Huu ni ugonjwa wa nguruwe unasababisha vidonda vyenye umbo la almasi kwenye ngozi (diamond shaped lesions)
NB: Minyoo ni miongoni mwa vitu vinavyosumbua sana ukuaji wa nguruwe hivyo inashauriwa kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mi3.                             PIA HUSISAHAU KWAMBA TUNASAMBAZA VITABU VYA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI NA KITABU CHA BUSTANI ZA MBOGA NA MATUNDA  VITABU HIVI NI VYA KUKUONGOZA TOKA HUJUI,UJUE,JINSI YA KUFANYA NA UNAFANYAJE ILI UPATE MAFANIKIO.TENA TUNACHIMBA VISIMA VYA KARAVATI AMBAVYO VIMEBORESHWA ILI KUTUMIA MIFUMO YA KISASA KABISA YA KUTUMIA PAMPU ZA KUTUMBUKIZA NA ZA JUU.TUNATENGENEZA GREENHOUSE.KAMA KUNA MTU ANAHITAJI KISIMA PAMOJA NA GREENHOUSE KUNA BEI MAALUMU AMBAYO TUNAMPATIA.KWA MAELEZO ZAIDI.                        0784  999  995.      0654   768   400.

Soma na Hizi Hapa:

  • MAGONJWA YA NYANYA.MAGONJWA YA NYANYA DALILI NA UTHIBITI WAKE. 1.Dalili za madoa yatokanayo na bakteria hutokea kwenye majani, matawi na kwenye matunda ya nyanya.  … Soma Zaidi
  • KILIMO CHA MATIKITIKILIMO CHA TIKITI MAJI Utangulizi Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao h… Soma Zaidi
  • KILIMO CHA MIPAPAI.MUONGOZO WA UZALISHAJI WA PAPAI UTANGULIZI Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa… Soma Zaidi
  • UJENZI WA MABANDA BORA YA KUKU.KANUNI ZA MSINGI ZA UJENZI WA MABANDA YA KUKU WA NYAMA KUKU 1,000 - 10,000 (UFUGAJI WA KIWANGO CHA KATI) ...mwendelezo... [[ Kwa wajasiliamilia wenye … Soma Zaidi
  • UHITAJI NA UMUHIMU WA MAJI KWENYE KILIMO.UMUHIMU WA MAJI UNATUPEREKEA KUWEKEZA NGUVU ZETU KWENYE UCHIMBAJI WA KISIMA.     Asilimia 80 ya uhitaji mkubwa wa mazao mengi ni m… Soma Zaidi

3 comments:

Jiunge Nasi Facebook

Zilizosomwa Zaidi

Pages

Powered by Blogger.