MUONGOZO WA UZALISHAJI WA PAPAI
UTANGULIZI
Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.
KUHUSU MPAPAI
Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu
i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya)
Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.
Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI
Miche ya mpapai
Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: -
1. Mbegu za Kawaida (Local seeds)
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.
2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaoja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1, MALAIKA F1 n.k.
Upandaji
Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.
Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.
Kitalu cha mipapai
BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5.
Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi.
Kiaisi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda. Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yalioja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu.
Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI WA SHAMBA
Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba.
Nafasi
Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.
Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.
NB: Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekari ( 400 hadi 800 kwa ekari)
Kupanda mimea shambani
Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.
shamba la mipapai
Uwekaji wa mbolea.
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbole gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phospate kwa kaisi kikubwa. Mfano; - 12:24:12. (NPK)
Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK)
Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.
Umwagiliaji
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji niya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.
Magugu
Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.
HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI
Kitalu - Wiki 1 - 6
Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa shamba - wiki 7 -16
Maua na kuweka matunda - wiki 17 - 21
Kukua kwa matunda - 22 - 26
Mavuno ya kwanza - Wiki 37 nakuendelea. KWA MAHITAJI YAKO YA MBEGU HIZI ZA KISASA WASILIANA NAMI KWA NAMBA HIZO CHINI.KWA WA MIKOANI TUNAWASAFISHIA. HUSISAHAU PIA KUNUNUA VITABU VYETU CHA BUSTANI ZA MBOGA NA MATUNDA PIA CHA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI PAMOJA NA UCHIMBAJI WA KISIMA CHA KARATI NA UTENGENEZAJI WA GREENHOUSE. 0784 999 995. 0654 768 400.
Monday, 2 May 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Jiunge Nasi Facebook
Zilizosomwa Zaidi
-
KILIMO CHA TIKITI MAJI Utangulizi Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wa...
-
Kilimo Cha Greenhouse Na Aina Zake. Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti...
-
MAGONJWA YA NYANYA DALILI NA UTHIBITI WAKE. 1.Dalili za madoa yatokanayo na bakteria hutokea kwenye majani, matawi na kwenye matunda ya ny...
-
MAEMBE NI UTAJIRI MKUBWA Waswahili husema eti rizizki ya Mbwa ipo miguuni mwake,usemi huu unamaana kuwa riziki ya mtu ipo katika nafasi ali...
-
KANUNI ZA MSINGI ZA UJENZI WA MABANDA YA KUKU WA NYAMA KUKU 1,000 - 10,000 (UFUGAJI WA KIWANGO CHA KATI) ...mwendelezo... [[ Kwa wajasilia...
-
MUONGOZO WA UZALISHAJI WA PAPAI UTANGULIZI Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili l...
-
UMUHIMU WA MAJI UNATUPEREKEA KUWEKEZA NGUVU ZETU KWENYE UCHIMBAJI WA KISIMA. Asilimia 80 ya uhitaji mkubwa wa mazao mengi ni maji na moj...
-
UFUGAJI WA NGURUWE Nguruwe ni mnyama asiecheua na mwenye kwato zilizogawanyika. AINA ZA NGURUWE (BREED) i) Largewhite -Rangi nyeupe -Ma...
-
TANGAZO TANGAZO TANGAZO. ILE KAMPENI YA UFUNDISHAJI WA BUSTANI ZA NYUMBANI NYUMBA KWA NYUMBA BADO INAENDELEA. ELIMU HII TUNAIFANYIA NYUM...
-
UFUGAJI WA SAMAKI. 1.Mambo yakuzingatia wakati wakuchagua eneo kwaajili ya ufugaji samaki. I. Aina ya udogo: hili nijambo muhimu kwani ain...
Makala Zilizopita
Pages
Powered by Blogger.
je vp kuhusu masoko kwani mkuliwa aanapo lima hutakiwa kua nasoko nje ili kukuza biashara
ReplyDelete