Tuesday, 31 May 2016

UFUGAJI WA SAMAKI.

UFUGAJI WA SAMAKI.

1.Mambo yakuzingatia wakati wakuchagua eneo kwaajili ya ufugaji samaki.
I. Aina ya udogo: hili nijambo muhimu kwani aina ya udogo huathiri kwenye kuchagua aina gani ya bwawa litumike. Tambua kuwa kuna aina nyingi ya mabwawa kama bwawa la udogo tupu (earthen pond) na bwawa la zege (concrete pond). Bwawa la zege hutumia gharama nyingi kulijenga ukilinganisha na bwawa la udogo tu. Hivyo ili bwawa liwe la udogo ni lazima aina ya udogo wa eneo husika uwe na sifa ya kutunza maji.
II. Maji: samaki huishi kwenye maji hivyo nilazima uwahakikishie upatikanaji wa maji safi na salama kwa uhai wao. Maji yawe yanapatika kwa Wingi, Salama na yenye kuweza kuwekwa katika miundombinu sahihi kwaajili ya kutumika wakati wowote. Maji yanaweza kuwa ya kisima, mto, ziwa, chemchem,au bomba. Kila aina ya maji ina faida zake na changamoto zake. Kwa mfano wakati maji ya mto huwa yanaweza kupatikana kwa urahisi lakin yanachangamoto yakuweza kukuletea vijidudu vya magonjwa kama minyoo, typhoid na kipindupindu.
III. Vifaranga: usishangae! Ndiyo mbegu za samaki yaani samaki wadogo huitwa vifaranga. Nilazima ujihakikishie upatikanaji wa mbegu bora kwaajili ya matokeo mazuri. Mbegu duni huchukua muda mwingi kukuwa na hivyo kumuongezea mkulima gharama za ufugaji na kumpunguzia kipato.
IV. Chakula: ufugaji wa samaki kwaajili ya biashara humuitaji mkulima kuwapatia samaki chakula za ziada (supplementary feed) ili samaki wakue kwa haraka zaidi. Kumbuka ukuwaji wa samaki hutegemea UBORA WA MAJI + UBORA WA CHAKULA.
V. Ulinzi na usalama:  ni vyema mkulima kuepukana na migogoro yeyote kama ya umiliki wa ardhi na matumizi ya maji ili kuondoa uwezekano kukuhujimiwa katika mradi wake.
VI. Usafiri: kwa nyakati tofauti mkulima atahitajika kusafirisha ima malighafi zitumikazo kwenye ufugaji au mazao ya ufugaji baada ya kuvuna. Hivyo ni muhimu kuzingatia uwezekano wa usafiri sahihi wakati wote. Usafiri siyo mtu awe na gari hapana ila uwepo wa miundombinu safi yaweza tosha.
VII.Soko: Mwisho wa ufugaji ni kuuza mazao yako kwa faida hivyo ni vyema mkulima akafanya tafiti za kupata soko la uhakika kwa mazao yake. Mkulima huweza tumia soko la karibu kama majirani na wafanyabiashara wa karibu. Pia anaweza kutumia soko la mbali.

Ufugaji wa samaki unalipa endapo tu mkulima atapata mtaalamu sahihi na akazingatia kanuni za ufugaji.

itaendelea.........................

Soma na Hizi Hapa:

  • UHITAJI NA UMUHIMU WA MAJI KWENYE KILIMO.UMUHIMU WA MAJI UNATUPEREKEA KUWEKEZA NGUVU ZETU KWENYE UCHIMBAJI WA KISIMA.     Asilimia 80 ya uhitaji mkubwa wa mazao mengi ni m… Soma Zaidi
  • KILIMO CHA MIPAPAI.MUONGOZO WA UZALISHAJI WA PAPAI UTANGULIZI Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa… Soma Zaidi
  • MAGONJWA YA NYANYA.MAGONJWA YA NYANYA DALILI NA UTHIBITI WAKE. 1.Dalili za madoa yatokanayo na bakteria hutokea kwenye majani, matawi na kwenye matunda ya nyanya.  … Soma Zaidi
  • KILIMO CHA MATIKITIKILIMO CHA TIKITI MAJI Utangulizi Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao h… Soma Zaidi
  • KILIMO CHA TIKITI MAJI.UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION UTANGULIZI Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya he… Soma Zaidi

0 comments:

Post a Comment

Jiunge Nasi Facebook

Zilizosomwa Zaidi

Pages

Powered by Blogger.