Thursday, 28 April 2016

KILIMO CHA TIKITI MAJI.

UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION
UTANGULIZI
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua : kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa.
UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.
UPANDAJI
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.
MATANDAZO (MULCHES )
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea za viwandani aina ya NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana. Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
UMWAGILIAJI
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.
Hii hufanywa kwa , kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.
MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.
UVUNAJI MATIKITI
Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;
Rangi ya mng’ao hupotea
Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.
Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
Soko la matikiti maji
Ukubwa wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja limekuwa likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti dogo mpaka 3000 kwa tikiti kubwa katika masoko.
Mavuno
Mavuno ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya
TANI 15-36 kwa hekta moja.

kwa ushauri wa kitaalamu.tuwasiliane.0784 999 995.     0654  768  400.

Soma Zaidi Hapa →

Wednesday, 27 April 2016

UFUGAJI WA NGURUWE.

UFUGAJI WA NGURUWE
Nguruwe ni mnyama asiecheua na mwenye kwato zilizogawanyika.

AINA ZA NGURUWE (BREED)
i) Largewhite
-Rangi nyeupe
-Masikio yao yamesimama wima
-Wana miili mikubwa
-Ni wazazi wazuri
-Hutoa nyama nzuri
ii) Landrace
-Rangi nyeupe
-Masikio yao yamelalia mbele
-Mwili mrefu
-Wana nyama nzuri
-Ni wazazi wazuri
iii) Saddleback
-Rangi nyeupe na baka jeusi mgongoni au rangi nyeusi na baka jeupe mgongoni
-Wana masikio yaliyolala
-Ni wazazi wazuri
-Wanatoa nyama nzuri

FAIDA ZA NGURUWE KWA UJUMLA
-Hutoa nyama nyeupe ambayo ni nzuri sana kwa binadamu
-Ni rahisi kutunza kwani wana uwezo wa kula mabaki ya vyakula
-Huzaa kwa wingi na kwa muda mfupi
-Hutoa mbolea kwa ajili ya kilimo
-Hutoa mafuta kwa ajili ya kupikia n.k

AINA ZA UFUGAJI
-Ufugaji wa ndani
Nguruwe hufugiwa kwenye banda tu 100% bila kutoka nje
-Ufugaji wa nje
Nguruwe kufugiwa nje kwa muda mwingi 70%-80%
-Ufugaji wa ndani na nje
Nguruwe kufugiwa ndani ya banda na nje kwenye uzio/fence @50%.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE
-Upatikanaji wa soko kwa ajili ya mazao ya nguruwe
-Aina ya nguruwe unaotaka kufuga kulingana na lengo
-Mtaji kwa ajili ya kuendesha mradi
-Eneo zuri la kuwafugia
-Upatikanaji wa chakula cha kuwalisha
-Utaalamu

VYAKULA VYA NGURUWE NA ULISHAJI
Utunzaji na ulishaji wa nguruwe  umegawanyika katika makundi
-Nguruwe wadogo/watoto
-Nguruwe wanaokua
-Nguruwe wenye mimba
-Nguruwe mzazi au anaenyonyesha
-Nguruwe dume
VIINI LISHE VINAVYOTAKIWA KWENYE CHAKULA CHA NGURUWE
-Wanga (kuupa mwili nguvu)
Pumba za mahindi au mpunga
-Protini (kujenga mwili)
Mashudu aina zote na unga wa dagaa
-Madini
Chokaa, chumvi na pigmix/pigboost
-Vitamini
Majani au mbogamboga
-Maji ni muhimu sana kwa kila kiumbe hai
BAADHI YA MAGONJWA  YANAYOWAPATA NGURUWE NGURUWE
i) African Swine Fever (homa ya nguruwe)
Huu ni ugonjwa hatari sana kwa nguruwe unaosababishwa na virus
ii) Swine dysentery
Huu ni ugonjwa wa kuhara husababishwa na bacteria aitwae treponema hyodyseteriae
iii) Respiratory disease
Ugonjwa wa mapafu
iv) Sarcoptic mange
Ugonjwa wa ngozi husababishwa na mangemites
v) Calibasilosis
Kwa nguruwe wadogo husababishwa na E.coli bacteria
vi) Coccidiosis
Kwa nguruwe wadogo
vii) Erysipelas
Huu ni ugonjwa wa nguruwe unasababisha vidonda vyenye umbo la almasi kwenye ngozi (diamond shaped lesions)
NB: Minyoo ni miongoni mwa vitu vinavyosumbua sana ukuaji wa nguruwe hivyo inashauriwa kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mi3.                             PIA HUSISAHAU KWAMBA TUNASAMBAZA VITABU VYA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI NA KITABU CHA BUSTANI ZA MBOGA NA MATUNDA  VITABU HIVI NI VYA KUKUONGOZA TOKA HUJUI,UJUE,JINSI YA KUFANYA NA UNAFANYAJE ILI UPATE MAFANIKIO.TENA TUNACHIMBA VISIMA VYA KARAVATI AMBAVYO VIMEBORESHWA ILI KUTUMIA MIFUMO YA KISASA KABISA YA KUTUMIA PAMPU ZA KUTUMBUKIZA NA ZA JUU.TUNATENGENEZA GREENHOUSE.KAMA KUNA MTU ANAHITAJI KISIMA PAMOJA NA GREENHOUSE KUNA BEI MAALUMU AMBAYO TUNAMPATIA.KWA MAELEZO ZAIDI.                        0784  999  995.      0654   768   400.

Soma Zaidi Hapa →

Tuesday, 26 April 2016

KILIMO CHA MATIKITI

KILIMO CHA TIKITI MAJI
Utangulizi
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
Tikiti maji ni moja ya mazao ya matunda ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa kote ulimwenguni. Zao ili ni moja ya mazao ambayo ni rahisi sana kuzalisha na lisilohitaji gharama kubwa. Gharama ya kulima ni kuweza kufahamu mazingira yanayofaa kwa ajili ya tikiti maji, uchaguzi sahihi wa mbegu, upandaji, matunzo na mambo mengine machache yasiyokuwa na gharama kwa mkulima.
Faida ni kubwa kwa mkulima, kwa kuwa zao hili huuzwa kwa kilo na ukubwa hutegemeana na matunzo shambani. Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa. Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.
Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;kawaida ekari1=sqm4000 Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3. Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500.
So ukishusha hesabu hapo juu:
Jumla ya mashina ktk ekari1 ni
Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000
Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000
Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs
18,000,000/=
Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!anza kulima zao hili ili uweze kujiongezea kipato na kuondokana na umaskini wa kujitakia. Amka sasa.
Aina
Kuna aina kuu mbili za matikiti maji, ambazo ndani yake zimegawanyika kulingana na aina ya mbegu, ilipofanyiwa utafiti na kuzalishwa. Aina hizo ni;
Matikiti yenye rangi ya kijani. Aina hii ni ya duara na huwa na umbo kubwa.
Matikiti yenye rangi ya mabaka mabaka. Aina hii ni ndefu na huwa na umbo la wastani.
Uzalishaji
Kwa kawaida ekari moja huchukua miche elfu mbili na mia tano (2,500) ya matikiti maji. Gharama ya uzalishaji wa zao hili ni ndogo sana ukilinganisha na aina nyinginezo za mazao. Tunda la tikiti maji huwa na uzito wa kati ya kilo mbili mpaka kilo kumi na tano. Kilo moja huuzwa kati ya shilingi za kitanzania 350-1000. Zao hili husaidia katika udhibiti wa magugu shambani, pamoja na utunzaji wa udongo kwa kuwa hutambaa na kufunika udongo.
Matayarisho ya shamba na upandaji
Baada ya kuchagua aina ya mbegu unayohitaji kupanda, inashauriwa kulima shamba na kuacha kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda miche yako ya matikiti.
Hakikasha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika, udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini. Hakikisha kuwa shamba lako lina nafasi ya kutosha kwa kuwa matikiti huhitaji nafasi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kupata mwanga wa jua wa kutosha. Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Kila shimo hakikisha umeweka mbegu tatu na uzipande kwa utaratibu wa pembe tatu au kwa lugha rahisi mafiga.
Zikishaanza kutoa matunda hakikisha kila shina unaacha matunda matatu mengine kata ili kuruhusu ukuaji mzuri wa tunda kwani yakiwa mengi yatakuwa yanagawana chakula hivyo tunda kuwa dogo ambalo ukipeleka sokoni unapata pesa kidogo.
Hali ya Hewa
Kabla ya kupanda hakikisha kuwa udongo una joto la wastani wa nyuzi joto 70°C. Unaweza kupanda kwa kutumia jembe la mkono au reki. Fukia mbegu kwenye mashimo kwa kutumia udongo laini na shimo lisiwe na kina kirefu, liwe na wastani wa inchi 1, ili kutoa urahisi kwa mbegu kuota. Kwa kawaida tikiti hupandwa kwa mstari mmoja kwenye tuta lenye mwinuko wa inchi 6 na upana wa futi 4. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimita 120.
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua: kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
Matandazo (Mulches)
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
Uwekaji Wa Mbolea
Mbolea za viwandani aina ya NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana. Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
Umwagiliaji
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
Matikiti hustawi na kuwa na kiwango kizuri cha uzalishaji katika ukanda wa joto. Kwa kawaida matikiti hayapendi sehemu yenye maji mengi. Zao hili huchukua takribani siku 75-90 tangu kupandwa hadi kuvuna. Hii hutegemeana na aina ya mbegu, hali ya hewa na utunzaji.
Maua Na Matunda
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.
Hii hufanywa kwa, kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.
Wadudu na magonjwa
Kwa kawaida zao hili halina wadudu na magonjwa mengi yanayolishambulia. Hii hutegemeana na uchaguzi sahihi wa eneo linalofaa kwa kilimo cha zao hili pamoja na hali ya hewa. Pamoja na hayo kuna baadhi ya wadudu ambao wamezoeleka katika zao hili.
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.
Vidukari: Wadudu hawa ni moja ya wadudu waliozoeleka kwenye matikiti, hushambulia sana zao hili na mara nyingi wasipodhibitiwa mapema Kabla ya kupanda hakikisha kuwa udongo una joto la wastani wa nyuzi joto 70°C. Unaweza kupanda kwa kutumia jembe la mkono au reki. Fukia mbegu kwenye mashimo kwa kutumia udongo laini na shimo lisiwe na kina kirefu, liwe na wastani wa inchi 1, ili kutoa urahisi kwa mbegu kuota.
Kwa kawaida tikiti hupandwa kwa mstari mmoja kwenye tuta lenye mwinuko wa inchi 6 na upana wa futi 4. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimita 120.
Ugonjwa
Zao hili hushambuliwa zaidi na ugonjwa wa Ubwiri unga. Ugonjwa huu ni hatari sana na usipodhibitiwa mapema kwa kuwa hushambulia majani ya mmea, husababisha mmea kufa baada ya muda mfupi jambo ambalo huathiri mavuno.Ni vigumu sana kuzalisha zao hili wakati wa msimu wa mvua, hivyo inashauriwa kupanda wakati wa kiangazi. Hali hii itasaidia mazao haya kustawi vizuri, ikiwa ni pamoja na kuepuka matunda kuoza kutokana na mvua kuwa matunda ya tikiti hukaa chini kwenye udongo.
Uvunaji Matikiti
Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;
Rangi ya mng’ao hupotea
Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.
Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
Matumizi
Matunda ya tikiti maji mara hutumika kwa kuliwa kama tunda ambapo watu wengi hulitumia sana majumbani, pamoja na kutengenezea vinywaji kama vile juisi, ambapo husindikwa na kutengeneza hiyo juice n.k. Lakini pia tunda hili hutumika kama dawa kwa baadhi ya maeneo ambapo majani yake,mizizi na tunda hutumika kutengenezea hizo dawa.
Soko
Tikiti maji ni moja ya mazao yenye soko kubwa na lisilotetereka. Soko kubwa ni kwenye mahoteli, viwanda vinavyotengeneza vinywaji baridi, pamoja na watu binafsi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Kwa sasa hapa Tanzania soko kubwa la matunda haya liko kwenye kampuni ya Bakhresa anayetumia matunda kutengeneza juice hivyo ukiwa nayo mengi ujue una uhakika wa soko.
Faida za matikiti maji
Tikiti maji ni tunda ambalo linapendwa sana na watu wengi duniani. Tunda hili limekuwa maarufu sana duniani kutokana na umuhimu wake kwa afya na mwili wa binaadamu.
Waingereza huliita tunda hili kwa majina mawili ambayo ni watermelon na milkmelon. Huko nchini India pia tunda hili hutumika sana na kuna aina mbili ambazo ni watermelon (Citrullus vulgaris) na milkmelon (Cucumis melo). Hapa kwetu Tanzania tunatumia sana aina moja ya tikitimaji ambayo ni watermelon (Citrullus vulgaris).
Tunda hili lin faida lukuki ambapo moja ni chanzo cha protini mafuta, nyuzinyuzi, wanga, madini ya calcium, chuma, phosphorus, vitamin A, B6, C, potassium, magnesium na virutubisho vingine vingi.
Pia kama tulivyoona hapo juu kuwa tunda hili ni chanzo cha vitamin A hivyo husaidia kuboresha uhai wa macho na kuondoa sumu mwilini.
Vitamin C inayotokana na tunda hili inasaidia kutia kinga mwilini, kuponya majeraha, kukinga uharibifu wa seli za mwili na kuboresha afya ya fizi na meno.
Wakati vitamin B6 itokanayo na tunda hili husaidia ubongo kufanya kazi vizuri na pia inasaidia kuibadilisha protini kuwa nishati.
Ukila tunda hili pamoja na mbegu zake unaondoa tatizo la upungufu wa mbegu za kiume kwani husaidia kuamsha hisia za kimwili, lakini pia huamsha hisia kwa watu wote hivyo badala ya kutumia vidonge kutibu tumia hili tunda.
Tikitimaji pia kutokana na asili yake ya kuwa na maji mengi, lina uwezo wa kusafisha figo pamoja na njia ya mkojo na kulainisha vizuri mishipa ya damu ili mzunguko wake uwe mzuri.
Tunda hili pia husaidia kupunguza uzito wa mwili na ugonjwa wa kisukari. (Diabetes).

KWA MAELEZO ZAIDI TAFUTA KITABU CHETU CHA KILIMO CHA BUSTANI ZA MBOGO MBOGA NA MATUNDA.

PIA KITABU CHA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.

KUJUA BEI NA NAMNA YA KUVIPATA PIGA SIMU ZIFUATAZO.
PIA TUNATOA HUDUMA YA KUCHIMBA VISIMA VYA KARAVATI AMBAVYO TUNAWEKA MIFUMO YA KISASA KWA KUTUMIA BELA PAMOJA NA PAMPU.    KWA WALE WANAOHITAJI GREENHOUSE PIA WATUONE.TUNAWEZA KUKUTENGENEZEA GREENHOUSE PAMOJA NA KISIMA KWA BEI NAFUU SANA.HUSISITE KUTUTAFUTA KWA NAMBA HIZO HAPO ILI KUJUA YALIYOFICHIKA.PIGA AU TUMA SMS UTAJIBIWA HARAKA.
0784 999 995.

0654 768 400.

Soma Zaidi Hapa →

Sunday, 17 April 2016

VITABU VITABU VITABU VITABU

VITABU  VITABU VITABU VITABU.

KWA WALE WAKULIMA HUU NI MSIMU WA KILIMO.

KUNA WENGI HAWAJUI NI KITU GANI SAHIHI CHA KULIMA MSIMU HUU.

KITABU CHA BUSTANI ZA MBOGA NA MATUNDA KITAKUFAA KUKUONGOZA KUFANIKISHA  KILIMO CHAKO TANGU KUANDAA SHAMBA MPAKA KUVUNA.

UTAKUTANA NA KILIMO CHA NYANYA,BIRINGANYA,MATIKITI,KITUGUU,PILIPILI,MAPAPAI,NK.

SAMBAMBA NA HICHO KIPO KITABU CHA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.

ILI KUJUA BEI NA NAMNA YA KUVIPATA PIGA  AU SMS.

HUSIULIZE HAPA.BALI ULIZA KWENYE HIZI NAMBA ILI UPATE MAJIBU HARAKA.

0784  999 995.

0654 768 400.

Soma Zaidi Hapa →

Thursday, 14 April 2016

OFA MAALUMU YA KUCHIMBIWA KISIMA.

OFA  MAALUMU YA KUCHIMBIWA KISIMA.

KUTOKANA NA  MAOMBI YA WAHITAJI YA WATU WANAOHITAJI KISIMA TUMEONA TUTOE OFA MAALUMU YA KUCHIMBIWA KISIMA.

TUNATOA OFA MAALUMU KWA WATU AMBAO WATAHITAJI KUCHIMBIWA KISIMA KATIKA JIJI LA DAR,MKOA WA PWANI,MOROGORO NA TANGA.

TUNATOA HUDUMA ZA AINA ZIFUATAZO KWENYE OFA HII.

1.TUNAKUTENGENEZEA KARAVATI.
2.TUNAKUCHIMBIA KISIMA CHA UREFU WA FUTI 75.
3.UKIWA NA PAMPU PAMOJA TANKI LAKO TUTAKUUNGANISHIA MIFUMO YA MAJI.

HUDUMA HIZI TUTAZITOA KWA GHARAMA NDOGO YA MILIONI 2.5.

KUMBUKA KISIMA HIKI NI KISIMA CHA KIENYEJI LAKINI UTENDAJI WAKE NI KISASA.

KISIMA HIKI KINADUMU MIAKA ZAIDI YA 300.

KWA MAWASILIANO YA KUPATA HUDUMA HII.

0784  999 995.

0654 768 400.

Soma Zaidi Hapa →

KILIMO CHA GREENHOUSE.

Kilimo Cha Greenhouse Na Aina Zake.
 Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.
Greenhouse(Banda Kitalu):  ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.
Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti  kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi.
Faida za Greenhouse
1.     Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
2.     Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao.
3.     Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha  mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
4.     Uwezo wa kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,  ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei ya juu na
5.     Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
6.     Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti  wake  ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
7.     Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili  ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
8.     Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture). Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi  wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea

Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha  Greenhouse.
·        Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani  ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga,  pamoja na nyanya. Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo  hazilimwi kwingine. Mazao maarufu  yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.
·        Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa  teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)
·        Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa  nchi ya Israel eneo lake ni kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse. Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.
·        Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao yanya na tango yanalimwa kwenye green house. Misri  10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote duniani. Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse.  Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama  Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).
Aina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:
1.     Aina za Greenhouse kwa  kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu
·        Quonset Greenhouse
·        Saw tooth type
·        Even span type greenhouse
·        Uneven span type greenhouse
2.     Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
·        Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
·        Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)
3.     Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
·        Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
·        Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
·        Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma
4.     Aina za Greenhouse kwa kigezo aina ya zana za ufunikaji (covering types)
·        Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (glass)- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani   greenhouse
·        Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)
5.     Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa
·        Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
·        Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
·        Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20).
KWA KUANZA KUWAONDOA HOFU MLIYONAYO TUMEWALETEA VITABU VYA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI NA KILIMO CHA BUSTANI ZA MBOGA MBOGA NA MATUNDA.
VITABU HIVI TUMECHUKUA YALE MASOMO TUNAYOFUNDISHA KWENYE SEMINA ZETU KWA GHARAMA KUBWA.
SASA TUMETENGENEZA VITABU HIVI KAMA SEMINA ISHIRINI TUKAZIWEKA PAMOJA NA KUKUUZIA KWA GHARAMA NDOGO SANA ILI UJUE JINSI YA KUANZA NA KUSONGA NAYO.
SOMA HAPO CHINI UJUE BAADHI YALIYOMO.AMUA LEO HUSINGOJE KESHO.
VITABU     VITABU     VITABU.
NITOE  MAELEZO KIDOGO JUU YA HIVI VITABU.
KWA WALE WATU WENYE NIA DHATI YA KUWA WAFUGAJI WA KUKU  WA KIENYEJI.
NA WALE WENYE NIA YA DHATI  YA KUWA WALIMAJI WA BUSTANI ZA MBOGA MBOGA NA MATUNDA.
HIVI VITABU SIO VITABU VYA KAWAIDA VIMEANDALIWA MAALUMU ILI KUONDOA MATATIZO MAZIMA KATIKA NYANJA HIZI.
MFANO.KWENYE KITABU CHA UFUGAJI WA KUKU MAMBO AMBAYO UTAFAIDIKA NAYO.
(1).JINSI YA KUANDAA MBEGU BORA YA KUKU WEWE MWENYEWE.
(2).KUANDAA VYAKULA VYA  VIFARANGA WEWE MWENYEWE.
(3).KUJUA MAGONJWA MBALI MBALI YANAYOWASUMBUA VIFARANGA NA KUKU.
(4).KUJUA DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU VIFARANGA NA KUKU.
(5).KUJUA AINA YA MAGONJWA MBALI MBALI NA TIBA ZAKE.
(6).KUJUA NAMNA YA KUTENGENEZA MABANDA BORA YA KUKU.
(7).KUJUA NAMNA YA KUTENGENEZA CHAKULA LISHE NA MCHANGANYO WAKE.NK.
KWENYE KITABU CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA.UTAJUA YAFUATAYO.
(1).NAMNA YA KUANDAA ENEO LA BUSTANI.
(2).KUJUA NAMNA YA KURUTUBISHA UDONGO.
(3).KUJUA NAMNA YA KUANDAA MBEGU BORA.
(4).KUJUA NAMNA YA KUTENGENEZA MBOLEA YA ASILI.
(5).KUJUA NAMNA YA KUBOLESHA USTAWI WAKO WA KIPATO NA AFYA YAKO.
(6).KUJUA NAMNA UNAVYOWEZA KUTAFUTA SOKO.NK.
BADALA YA KULIPIA SEMINA MOJA KWA GHARAMA KUBWA TUMEAMUA KUKULETEA VITABU HIVI AMBAVYO BAADA YA KUVINUNUA VINAUWEZO WA KUKUELEKEZA HATA KAMA UELEWA WAKO NI MDOGO NA UKAELEWA.
MARA BAADA YA KUVIPATA HUTOJUTIA HAKIKA.
WATU WA MIKOANI UKIHITAJI VITABU VYOTE VIWILI TUTAKUCHANGIA USAFIRISHAJI.
KWA MAELEZO YA KUJUA BEI NA NAMNA YA KUVIPATA WASILIANA NASI KWA NAMBA HAPO CHINI.
KISIMA KISIMA KISIMA KISIMA.
TUNACHIMBA KISIMA CHA KARAVATI.
VISIMA HIVI TUMEVIBORESHA KWA KUWEKA MIFUMO YA KISASA KATIKA MATUMIZI.
KWAHIYO KIMUONEKANO KINAONEKANA CHA KIENYEJI ILA KIUTENDAJI NI CHA KISASA.
KISIMA TUNAKUCHIMBIA KWA BEI NAFUU SANA NA HUWEZI PATA SEHEMU YOYOTE ILE.
KISIMA HIKI KINAFAA KWA MATUMIZI YOYOTE YALE.
KWA MFANO.
WATU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI,KWA MATUMIZI YA NYUMBANI,KWA BIASHARA YA KUUZA MAJI,WAFUGAJI WA KUKU,SAMAKI,NK.
BEI ZETU KWA UWIANO.
(1).TUNAKUCHIMBIA KISIMA,TUNAKUPATIA PAMPU NDOGO,TUNAKUPATIA TANKI LT 1000.
(2).TUNAKUCHIMBIA KISIMA,TUNAKUPATIA PAMPU NDOGO.
(3).TUNAKUCHIMBIA KISIMA TU.
WATU WA MIKOANI NA NCHI ZA JIRANI WAO WATAGHARAMIA KUTUSAFIRISHA NA HUDUMA ZOTE ZA MARADHI KWA MDA WOTE.
WATU WALIOPO DAR WAO WATAHUSIKA NA KUSAFIRISHA MASHINE ZETU ZA KUTENGENEZEA KARAVATI.
UTACHAGUA SASA WEWE UNATAKA HUDUMA IPI KISHA TUPIGIE SIMU AU SMS KWA NAMBA HIZI.GHARAMA ZETU NI NAFUU SANA.TUTAFUTE TAFADHARI.HATUWEZI KUTAJA BEI HAPA KWAKUWA BEI NIMATOKEO YA MAELEWANO.
PIA KWA WALE AMBAO WALIWAHI KUCHIMBIWA VISIMA VYA NAMNA HII VIKASHINDWA KUTOA MAJI NA UNA UHAKIKA MAENEO HAYO YANA MAJI.HUSIKOSE KUTUTAFUTA ILI TUMALIZE TATIZO HILO.
HUSINUNGUNIKE NA UNAPOTUONA TUNATANGAZA HUMU UNAANZA KUTULAANI.ULIKUTANA NA WABABAISHAJI WALIOVAMIA KAZI HISIYO YAO.
KAULI MBIU YETU.
TUPE KAZI ILI UTUAMINI.
MAWASILIANO HAYO.HUSHINDWE MWENYEWE.
HUNA HAJA YA KUTUMIA GHARAMA KUBWA KWA KUSHIMBA KISIMA WAKATI SISI WAZALENDO TUPOOOO.
TAHADHARI.MDA MWINGI NAKUWA SIPO MTANDAONI.ILI UPATE MAJIBU KWA HARAKA TUMIA HIZO NAMBA.
0784  999  995.
0654  768  400.
Soma Zaidi Hapa →

Jiunge Nasi Facebook

Zilizosomwa Zaidi

Pages

Powered by Blogger.